KARIBU

KARIBU SANA MTUMISHI WA MUNGU. KUNA MENGI YA KUJIFUNZA MAHALI HAPA. JISIKIE HURU KUTUMIA CHOCHOTE UTAKACHOKIPATA MAHALI HAPA. NA WEWE PIA UNAKARIBISHWA KUSHIRIKISHA WENGINE BARAKA MUNGU ALIZOKUPA. SHIRIKI PIA KATIKA KUSHAURI, KUONYA NA KUFUNDISHA ILI KANISA LA MUNGU YESU KRISTO LIZIDI KUSIMAMA. KARIBU SANA. KUMBUKA ENEO HILI HALIFUNGAMANI NA DHEHEBU LOLOTE BALI TUNAFUNGAMANA NA YESU KRISTO. BIBLIA NDIYO MAMLAKA KUU INAYOTUONGOZA KWA MAANA NDIYO NENO HALISI LA MUNGU.

Tuesday, May 14, 2013

RAIA WANNE WASAUDIA WALIOKUWA WANASHUKIWA KUHUSIKA NA ULIPUAJI WA MABOMU  ARUSHA WAMEACHIWA HURU.

Dubai - Three Emiratis arrested in Tanzania after a deadly attack on a church there a week ago have been freed and are back home, the Al-Khaleej daily reported on Monday.

Tanzanian authorities had arrested them "because they happened, by chance, to be at the site of the attack", the paper said, citing tweets of the United Arab Emirates foreign ministry.

The trio were released with the foreign ministry's help following "co-ordination between the UAE embassy and Tanzania", it said.

The report quoted "informed sources" as saying that the three Emiratis had returned home.

Saudi Arabia's foreign ministry announced Sunday that a Saudi citizen who had been arrested at the same time as the UAE nationals had been freed without charge.

The Saudi and the three Emiratis were arrested along with five Tanzanians after last Sunday's bombing, described by Tanzanian President Jakaya Kikwete as "an act of terrorism".

It was one of the worst such incidents to hit the east African country in years.

In addition to the three people killed in the blast, more than 60 people were injured when attackers hurled a bomb into the compound of the newly built Saint Joseph's Roman Catholic church.

The church was celebrating its inaugural mass at the time and was filled with worshippers.

- AFP

Tuesday, May 7, 2013

VURUGU ZA KIDINI TANZANIA



SABABU 10 KWA NINI SHAMBULIO LA ARUSHA NI LA KIDINI
Akihojiwa na shirika la utangazaji la BBC, Balozi wa Tanzania Uingereza Mh. Kalaghe alikataa kwa nguvu zote kwamba shambulio la Arusha lililosababisha vifo na majeruhi sio la kidini bali la kigaidi! Kwa muda mrefu watanzania tumeendekeza dhana  ya kutokuwa wakweli wala wawazi kwenye mambo yanayoamua mstakabali wa nchi yetu. Vuguvugu la udini Tanzania sasa linaadhimisha miaka 20 Tangu lilipoanza na mashambulizi dhidi ya mabucha ya Nguruwe. Na sasa balozi huyu amethibitisha kwamba watanzania hatutaki kuwa wakweli!!!
Hizi ni sababu 10 kwa nini Shambulio la Arusha ni la Kidini
1. kilichoshambuliwa ni IBADA! hivi kama washambuliaji walilenga mambo mengine si wangeshambulia mahali pengine na sio ibadani?
2. Walioshambuliwa ni WAKRISTO! kwa muda wa mwaka mmoja sasa tunauzoefu wa makanisa kuchomwa na viongozi wa dini kuuawa. Zanzibar kuna msiba na Geita kuna msiba! na sasa ARUSHA UMEKUWA MSIBA MKUBWA ZAIDI!
3. lililoshambuliwa ni kanisa KATOLIKI! ukianzia na kujeruhiwa na kuuawa kwa mapadri Zanzibar na kushambuliwa Arusha kanisa katoliki wamekuwa ni waathirika wakubwa kwa sababu ya IMANI ILIYOJENGEKA KWA WAISLAM KWAMBA KANISA KATOLIKI NDIYE ADUI WAO MKUBWA!
4. Yaliyoshambuliwa ni MAENDELEO! Kwa miaka mingi kanisa limekuwa likishindana katika kuleta maendeleo na waislam wamekuwa wakishindana katika kusoma Quran! Leo waislam wanalalamika kwamba wakristo wanapendelewa! BADALA YA WAO KULETA MAENDELEO WANAAMINI KATIKA KUHARIBU MAENDELEO YA WAKRISTO KWA MABOMU! wakati wakishambuliwa OLASITI walikuwa wanasherehekea kupandishwa daraja na kuwa parokia. Maana yake wanasonga mbele kwa maendeleo na mabomu hayatawarudisha nyuma.
5.Aliyeshambuliwa ni VATCAN! Mashambulio haya yalilenga kuliumiza kanisa katoliki. Bila shaka wangeanza na vatcan, wangefuata wajerumani(lutheran) na waingereza (Anglican) wangefuatia. Haya ni madhehebu yanayoongoza kwa kuwa na waamini wengi na vitega uchumi vingi na shuhuli nyingi za kijamii.
6. Waliokamatwa ni WAARABU! mpaka sasa raia wanne wa SAUD ARABIA wanashikiliwa. Kuna ugomvi wowote kati ya serikali na WASAUDIA? kama hakuna kwa nini wagombane na mtu asiye adui yako?
7.Aliyerusha bomu ni mkristo? kwa nini nimeuliza! kwa sababu mpaka sasa majina ya watu tisa hayatajwi ila linatajwa la mmoja mwenye jina la kikristo! akili haifunguki? kama wanne ni WASAUDIA je hao watano ni wana majina gani? kwa nini linalazimishiwa hilo moja?
8.kila Rais wa Tanzania akiwa ni muislam tarajia vurugu za waislam! ilitokea kwa Mwinyi na sasa kwa Kikwete lakini haikutokea kwa Nyerere wala kwa Mkapa
9. Zanzibar wanaamini kwamba, katika kutengeneza dola yao nje ya Muungano Ukristo ni tatizo kubwa. na sasa wanataka kuwatisha wakristo ili tuone kila vurugu inatokea zanzibar.
10.Baadhi ya waislam wameona ELIMU NI GHALI! kwa hiyo wameamua kujaribu UJINGA!

na wewe una la kuchangia? karibu!

Monday, April 1, 2013

IBADA YA UMOJA WA MAKANISA ARUSHA - MFANO WA KUIGWA



Kwa muda mrefu umoja wa madhehebu Arusha umekuwa ni mfano wa kuigwa. Ibada hii ya pamoja ya ijumaa kuu imedumu kwa miaka mingi. Kila wakati kama huu tofauti zote za kidhehebu huwekwa kando na kushuhudia umoja wa kipekee baina ya wachungaji na mapadri. Maaskofu wa makanisa mbalimbali hupata muda wa kutoa nasaa kwa waamini wao. Viongozi wa kisiasa hupata nafasi ya kusalimia wapiga kura wao. kwa hakika huu umoja unapaswa kudumishwa. Kama kawaida kitu chochote kizuri huwa hakikosi changamoto. Blog hii inapenda kutoa changamoto zifuatazo.
1. Kwa nini Umoja wa madhehebu ya kikristo Arusha hauna maono ya kununua vyombo vya mziki? kwa hakika kama kila mchungaji(kanisa) angechangia angalau 500,000 kwa mwaka naamini vingepatikana vyombo bora sana vya mziki. Kwa miaka nenda rudi changamoto ya vyombo vya mziki (PA) imekuwa sugu. wengi wa waamini ambao hawapo karibu na jukwaa kuu huwa hawapati mawasiliano vyema. Baba zetu hebu liangalieni hili.
2. Jukwaa. Kwa hali ya uwanja wowote wa mpira jukwaa kuu huwa halileti picha ya muunganiko kwa wasikilizaji. Ni vema jukwaa kuu likawekwa angalau katikati ya uwanja. Kwa nguvu ya umoja huu mkitushirikisha waamini wenu jamani hatushindwi kuchonga jukwaa bora na kubwa litakalohudumia ibada hii kwa namna ya kipekee.
3. Nyakati za nyuma tulizoea kuwa na mikutano ya injili inayohudumiwa na umoja wa madhehebu ya kikristo Arusha. Tafadhali fufueni enzi hizo ambako mikutano haikuwa kwa ajili ya kukua kwa dhehebu fulani bali kuuleta pamoja mwili wa kristo.
Je? wewe mmwenzangu una maoni gani ili umoja huu uzidi kusonga mbele?
Karibu utoe maoni yako na wewe!

Saturday, February 2, 2013

KARIBU CHRIST STUDIOS.
Unapoingia kwenye Blog hii kwa mara ya kwanza naomba ukutane na habari hii njema kwako. Kwa uzoefu wa miaka mingi nimefanya kazi ya kurekodi Mziki wa Injili na kwa neema ya Mungu nikapata kibali machoni pa watu wengi.
KWA NINI CHRIST STUDIOS?
Kwa wengi wanaonifahamu wangependa Studio iitwe kwa jina Langu ambalo wamelizoea. Lakini Studio hii si kwa ajili ya biashara tu bali mapato yake ni kwa ajili ya kueneza neno la Mungu. Nia na madhumuni yangu ni kwamba kutokana na ubora wa kazi tuzifanyazo, Kristo Yesu peke yake ndiye ainuliwa. Usipate shida wewe ukifika ARUSHA ulizia tu JOHN MTANGOO STUDIOS utafika.Lakini pia Lengo letu ni kuwapelekea vijana injili na hasa walioko Mashuleni  na Vyuoni. Ingependeza zaidi kwamba kila jambo jema juu yetu likinenwa basi kristo Yesu NDIYE ATAMKWE SANA!
WITO WETU.
Tunataka tuwe studio ya kisasa inayotoa kazi bora zenye kumtukuza Mungu.
MAONO YETU.
Maono yetu ni kuwafikia watu wengi kwa injili ya Yesu Kristo kupitia mziki.
KAZI TUZIFANYAZO.
Studio Yetu inafanya mlolongo wa kazi zifuatazo
- Kurekodi sauti (Audio Recording)
- Kurekodi Video (Video Recording)
- Kuandaa mziki (Music programming and arrangement).
- Kufundisha Sauti (Vocal Training).
- Shule ya mziki
- Kurekodi Mtangazo ya Biashara
- Kurekodi mahubiri
- Kuandaa vipindi vya redio
KAZI TULIZOFANYA.
Mungu ametupa Neema ya kuhudumu na vikundi vingi sana. Baadhi vimefanikiwa sana. Miongoni mwa waliofanikiwa baada ya kufanya kazi na sisi ni
- BEATRICE MUHONE (Ingoje Ahadi & Si njia Rahisi)
- JACKSON BENT (Si njia rahisi)
- MIRIAM lukindo (Asubuhi)
- TUMAINI (Shangilieni) KWAYA (Unishike & Nyimbo za matumaini) pamoja na LIVE RECORDING ya nyimbo za matumaini.
- MAMAJUSI KWAYA MOSHI - Majira ya jioni
- GODWIN OMBENI - Huyu Album zake zote pamoja na mpya ya Band yake amefanyia kwetu.
- IMANI KWAYA KKKT - KIPAWA Dar - es - salaam -- Hawa pia wamefanya na sisi Album zao za mwisho mbili. Usishangae kwamba tunapata na vikundi kutoka DAR, maana tumefanya kazi na kwaya nyingi sana Tanzania na Kenya.
MOBILE STUDIO
Dunia inaenda kasi sana. Maisha yamekuwa magumu na upatikanaji wa pesa ni changamoto isiyo na majabu. Kwa kutambua hili tuna studio inayokufuata mahali ulipo. Haijalishi ni kwaya ama mtu binafsi wewe tuambie tu na tutakufikia.

Kwa maelekezo zaidi tafadhali usisite kututebelea.
Tunapatikana
ARUSHA - Nanenane (njiro)
+255787416177 na +255766159501
Email:johnmtangoo@gmail.com